Na Magreth Chaba
Karagwe.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Karagwe wamemuomba waziri wa ujenzi
Daktari John Magufuli kumulika zoezi la ulipaji fidia kupisha ujenzi wa
barabara ya Kyaka – Bugene yenye urefu wa Km. 69.1 kwa madai kuwa uthamini wa
mali ulifanyika kwa upendeleo.
Wananchi wa vijiji vya Kihanga na Kishao walitoa malalamiko hayo
baada ya kubainika kwenye orodha ya watakaolipwa fidia zao nyumba zilizojengwa
miaka ya karibuni na nyumba zilizojengwa zaidi ya miaka 100 zikiondolewa
katika orodha ya kufidiwa.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kishao Clement Nsherenguzi (76)
alisema kuwa baadhi ya majirani walio na ardhi bila mazao katika eneo la mita
22.5 wamepewa fidia, na watu waliojenga hivi karibuni miaka michache wamepewa
ambapo aliongeza kuwa zoezi la tathimini na utoaji wa fidia limeghubikwa na
ahrufu ya huongo na rushwa.
“Sijui wanatumia vigezo na sheria gani katika kutoa fidia wazazi
wangu wameishi hapa tangu mwaka 1880 na baadhi ya mibuni ilipandwa. Mwaka 1920,
mimi mwenyewe nimezaliwa mwaka 1935 sasa naitwa mvamizi wa barabara mimi na
barabara nani mvamizi? Alisema Nsherenguzi.
Alisema kwamba, migomba yake 300 mibuni 50 vyenye thamani ya
shilingi 15,960,000/= viko kwenye orodha ya kufyekwa bila fidia ni pamoja na
kiwanja ploti EE. 35 alichogawiwa na Halmashauri ya wilaya ambacho kinampa kodi
kila mwaka katika eneo la Kayanga.
Naye mkazi wa kijiji hicho Magreth Peter (70) ambaye ni mama mjane
alisema ameelezwa na Tanroads mkoa wa kagera kuwa nyumba yake itabomolewa bila
fidia wakati huo jirani zake ambao wako ndani ya mita 22.5 kama yeye wakiwa
wameanza kulipwa.
Mwananchi mwingine wa kijiji hicho Adventina Furuka (69) ambaye
pia ni mjane alishangazwa na baadhi ya nyumba za kifahari zilizojengwa miaka ya
karibuni katika kijiji hicho kuonekana katika orodha ya watakaolipwa huku wao
majina yao yakikosekana.
“ Kwa mtindo huu rushwa katika nchi hii itatumaliza kama
waziri mwenye dhamana kama hataingilia haraka uthaminishaji uliofanyika katika
barabara ya Kyaka – Bugene inayojengwa kwa kipande cha lami Alisema furuka.
Pia waliowatuhumu walioendesha zoezi la utathimini baada ya
kudaiwa kuwataka wamiliki wa nyumba za zamani kupeleka uthibitisho wa
stakabadhi za kununua mabati ya kuezekea ili waingizwe kwenye orodha ya
watakaofidiwa.
Kwa upande wake mzee Joseph Lwiza alidai zoezi la uthamini lilijaa
mazingira yenye utata kwani baadhi ya wananchi waliitwa kwa ajili ya
majadiliano na walioendesha zoezi hilo.
Aidha alisema majirani zake walioko, kwenye mita zile wameanza
kupokea malipo huku yeye akijulishwa kuwa hatalipwa.
No comments:
Post a Comment