Saturday, March 24, 2012

MAUAJI YA ASKARI POLISI (W)BIHARAMULO

Na
Magreth Chaba
Biharamulo
WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wasiojulikana idadi mara moja wamemuua askari polisi katika machimbo ya Tulawaka katika eneo la Mavota Wilayani Biharamulo  kicha kumpora bunduki ikiwa na risasi zaidi ya 40 aliokuwa akitumia katika doria.
 Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Henry Salewi  amethibitisha kutokea kwa  tukio hilo  lilo tokea Machi 22, usiku wa kuamkia Machi 23, mwaka huu usiku.
Askari polisi aliyeuawa ametambuliwa kuwa ni PS konstebo  Dickson mwenye namba. G.2626 ambapo aina ya bundi alioporwa na watu hao ni Short gun mashine ambapo namba yake bado haijajulikana.
Kamanda Salewi alisema katika wauaji  hao walitumia chuma aina ‘Moke’ ambayo waliitumia kumtoboa nacho kichwani mara nne.
Alisema chuma hicho hutumika zaidi katika maeneo ya machimbo katika kuchimba ardhi.
Alisema siku ya tukio polisi huyo alikuwa na wenzake wanne ambapo kiutaratibu wakiwa malindoni hapo, huwagawanyika na hivyo kila mmoja kuangalia upande wake, ambapo kwa siku hiyo, wenzake waliingiliwa na shaka kwani hadi jana asubuhi hawakuweza kumwona akijitokeza.
Alisema kutokana na hali hiyo, walianza kumtafuta, ambapo walimkuta akiwa ameuawa kwa kutobolewa kichwani na chuma hicho mara nne.
Kamanda Salewi aliaeleza kuwa wauaji hao ni majambazi ambao jawajajulikana idadi hadi hivi sasa na haijaeleweka walikuwa na sialaha ya aina gani.
Alisema polisi hao walikuwa wakilinda ukuta wa jengo la machimbo la Tulawaka , ambapo mauaji hayo yalipomkuta askari huyo
Hata hivyo habari zaidi kutoka katika eneo la tukiko zinaeleza kuwa, watu waliohusika katika mauaji hayo ni Wachimbaji wadogo wa eneo hilo, siku ya tukio, Kostebo Dickson alienda kufanya doria usiku peke yake katika eneo hilo la machimbo lengo likiwa ni kuwazuia wachimbaji wadogo wanaojulikana eneo hilo kama Wangoni, ambao ni wavamizi wanaofahamika zaidi katiak eneo hilo kama wavamizi.
Kutokana na hali hiyo, haijaeleweka nia ya wangoni hao ilikuwa ni kutaka kumuua ama kumpora silaha.
Halikadhalika haijaeleweka kama costebo Dickson aliwataka watu hao wasiondoke na jiwe waliopata ama walitofautiana nini kati yao.
Kutokana na tukio hilo jana usiku wa kuamukia leo Jeshi la polisi lilitoa timu ya askari wapatao 40  wakiongozwa na baadhi ya maofisa wao kwenda katika eneo hilo la machimbo kufanya uchunguzi wa jambo hilo likiwa ni pamoja na kuwatafuta wauwaji na kuihakikisha linapata silaha ilioporwa ili isiweze kutumia mikononi mwa majambazi.
Tayari mwili huo umesafirishwa usiku wa kuamkia leo kwenda kwao Mkoani Rukwa  wilayani Sumbawanga kwa mazishi.
Katika machimbo la Mavota  ambayo yako ndani ya kijiji cha Mavota Kata Kiniha kinachomilikiwa na Kampuni ya Barrick  kumekuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya mauji, ambapo mara nyingi ni polisi kuuawa raia.
Mwaka 2009 polisi waliwauwa vijana watatu kwa kuwapiga kwa risasi kwa madai kuwa walivamia kituo cha polisi kwa kutaka kukiteketeza kwa moto, ambapo pamoja na mambo mengi ambayo yaharipotiwi hasa za mauaji wa raia yanapofanyiwa na polisi hao tetezi zilidai kuwa ni  vijana hao walienda kudai jiwe lao walionyang’anywa na polisi hao 

Wednesday, March 21, 2012

SHAHIDI AJIKAANGA MWENYEWE KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI

Na
Magreth Chaba

Shahidi wa pili katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu Jimbo la Biharamulo Magharibi Saniha Kasimu (23) mkazi wa Runazi wilayani Biharamulo akiongozwa na wakili wa upande wa mlalamikaji Bw. Aaron Kabunga shahidi huyo amekili kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa uchaguzi.

Mbele ya jaji wa mahakama hiyo Jaji Richard Kibera wakili wa serikali Bw. Pius Mboya, wakishirikiana na wakili wa serikali Bw. Isimaily Majoti na wakili wa upande wa wajibu maombi Bw. Mathias Rweyemamu shahidi huyo wa pili alikili kujihusisha na vitendo vya rushwa, udanganyifu wakati  wa uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani na kukipa ushindi Chama cha CHADEMA.

Shahidi huyo Bi. Kasimu ameieleza mahakama kuwa katika kipindi hicho cha uchaguzi yeye alishiriki kama mgombea udiwani viti maalum, Kata ya Runazi, kupitia chama cha CHADEMA, pia alikuwa wakala wa usimamizi wa wapigaji kura Kata ya Nemba kupitia CHADEMA na alikuwa Katibu wa vijana tawi Kata ya Runazi na alikuwa akihamasisha vijana wadogo kujiandikisha kupiga kura kwa kuwapa pesa.

Pia shahidi huyo amesema kuwa wakati wa kampeni alikuwa akihamasisha vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura katika mikutano ya hadhara na alishiriki kampeni za nyumba kwa nyumba huku akitoa fedha ili kuwashawishi wananchi waweze kukipigia kura Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Amevitaja baadhi ya vijiji ambako alifika na kutoa rushwa hiyo kuwa ni kijiji cha Nyambale Kata ya Lusahunga hakumbuki kiasi alichotoa na alikuwa akitoa sh. 50,000/= kwa wanawake na vijana sh. 30,000/= na kijiji cha Migango Kata ya Runazi ambako hakumbuki alitoa fedha kiasi gani.

Shahidi huyo Bi. Kasimu pia amekili kuvuruga uchaguzi mkuu 2010 kwa kuhamasisha vijana wadogo chini ya miaka (18) kujiandikisha, pamoja na kutoa rushwa kwa wananchi kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU na amekili kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Aidha, shahidi huyo katika ushahidi ameieleza mahakama kuwa alikuwa akitoa rushwa hizo mchana na usiku na ameamua kutoa ushahidi huo si kwa chuki bali ni kukilekebisha chama na kusahihisha makosa yote na kiwe katika mstari mzuri.  Na kuiomba mahakama imsamehe kwa makosa aliyoyatenda mwaka 2010 na yuko tayari kulipa faini ya makosa hayo.

Hata hivyo, shahidi huyo baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake alitiwa nguvuni na jeshi la polisi wilayani hapa.

Tuesday, March 20, 2012

KESI YA KUPINGA MATOKEO BIHARAMULO


Na
Magreth Chaba

Kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Biharamulo
Magharibi, iliyoanza kusikilizwa Machi 14, mwaka huu katika Mahakama
ya Wilaya Biharamulo na Jaji Richard Kibela.

Imeendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo leo, ambapo upande wa
watoa maombi mlalamikaji namba moja Bw. Oscar Lwegasira Mkasa na
mlalamikiwa Mbunge wa Jimbo hilo Bw. Anthony Mbassa pamoja na
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya ya
Biharamulo wameendelea kutoa ushahidi wao.

Akiwakilisha utetezi wake shahidi wa kwanza, Bw. Oscar Lwegasira Mkasa,
ambaye ni Mdai – akiongozwa na Wakili Aaron Kabunga mbele ya Jaji
Ridhard Kibela.

Shahidi huyo ameileza mahakama kuwa mnamo Oktoba 31-2010 katika
uchaguzi mkuu wa kitaifa, Rais, Bunge na Madiwani kuwa uchaguzi huo
katika Jimbo la Biharamulo Magharibi ulighubikwa na hira za makusudi,
Rushwa na udaganyifu.

Shahidi huyo ameileza mahakama kuwa, hila hizo zilifanywa na Chama cha
CHADEMA sambamba na Mawakala wake pamoja na tume ya Uchaguzi.
Kuandikisha watoto chini ya miaka 18, wapatao 2,325 walishiriki katika
zoezi la kupiga kura na kukipa ushindi Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA katika Jimbo hilo .

Aidha Shahidi huyo Bw. Mkasa amewakilisha maelezo 15 mbele ya Jaji wa
Mahakama hiyo Richard Kibela ambavyo vitatumika katika maombi ya kesi
yake.

Hata hivyo mahakama hiyo imetupilia mbali baadhi ya vielelezo baada ya
kusikiliza upande wa pili wa wajibu waombi ambao ulipinga kupokelewa
kwa baadhi ya vielelezo.

Vielelzo vilivyotupiliwa mbali na mahakama hiyo ni orodha ya majina ya
wapiga kura, fomu ya matokeo ya uchaguzi Kata ya Lunazi, Fomu ya
matokeo kituo cha Shule ya Msingi Kitwechembogo Kata ya Luziba
iliyodaiwa mahakamani hapo kuwa imeokotwa, Fomu kituo cha Kisuma,
(Kagondo stoo 2; na Kagondo mbili), ambavyo vituo havipo. (Vituo hivyo
vya Kagondo viko viwili kwa tofauti kama zilivyoainishwa).
kes hiyo imeahirishwa kusikilizwa hadi hapo kesho itakapo endelea kusikilizwatena huku upande wa mlalamika ukiendelea kutoa ushahidi wake.
 
 
 

Friday, March 2, 2012

TUTUNZE MAZINGIRA

                                                                                                    


Baadhi ya wananchi wakifanya  usafi katika mazingira ya makazi yao kutokana na utupaji wa taka ovyo unao changia uharibifu wa mazingira na kuharibu uoto wa asili





Mazingira ni vitu vyote vilivyopo katika uoto wa asili ikiwa ni pamoja na wanyama ,mimea, maji wadudu na udongo, kuwa vitu hivi vyote vina sitahili kuhifadhiwa ili kutunza mazingira.

Hifadhi ya mazingira katika maisha ya binadamu ni jambo la msingi  viumbe hai wanategeneza maisha yake kutokana na ubora wa uhifadhi wa mazingira, rangi ya umbijani katika mazingira huvutia na kuongeza ubora wa hewa safi kwa viumbe hai.

Jamii nyingi hapa nchini wameshindwa kuhifadhi mazingira kutokana na  kuwepo kwa nishati duni kwani wananchi hukata miti ovyo uchomaji wa mistu na hali hiyo imesababisha uharibifu wa mazingira kwani asilimia 80 wanaishi vijijini ambako hakuna nishati mbadala.

Uharibifu wa mazingira umechangia kuporomoka kwa uchumi kutokana na sehemu kubwa ya nchi kuwa jangwa jambo ambalo huchangia uzalishaji kuwa duni .

Aidha vitu vingine vinavyo changia uharibifu wa mazingira ni viwanda vingi kujengwa katikati ya makazi ya watu na kuchangia kuwepo kwa hali ya ukaa na kuathiri hali ya hewa na Afya za binadamu,ni pamoja na baadhi ya jamii za kitanzania kufuga mifugo wengi ambao nao pia huchangia uharibifu wa mazingira kwa kusababisha mmomonyoko wa udongo.




EIYEMBE LYETAABA

kijana mmoja ambaye pia ni mwandishi wa habari akijari namna ya kuvuta tumbaku kwenye kiko maarufu kama ( Eiyembe lyetaaba)kwa watu wa mjini bukoba (ABAHAYA) picha na Magreth  Chaba

Thursday, March 1, 2012

TUDUMISHE MILA ZETU TUACHANE NA MILA ZA KIGENI

Katika kudumisha mila na tamaduni zetu hizi ni baadhi ya ngoma za jadi  zilizotumika na zinaendelea kutumika  katika utamaduni mwa mwafrika katika kudumisha mila na desturi hutumika wakati wa sherehe, matukio ya hatari na katika mikutano na awali zititumika kuwa burudisha machifu .

Ngoma hizo hupatikana katika miji ya watu binafsi ,ofisi za vijiji na katika majumba ya makumbusho mbalimbali yaliyopo hapa nchini kama vile BUDAP iliyopo eneo la Nyamkazi  Bukoba Mjini,Bwera nyange Wilayani Karagwe ,Kiyanja, Kiziba, Kyamtwara Bujora Mwanza na sehemu nyinginezo hapa nchini  zilizo kuwa ni Makao Makuu ya Machifu.

Tamaduni hizi zinapaswa kuendelezwa kwani jamii nyingi zimeanza kudharau tamaduni na kushabikia tamaduni za kigeni, kwani ngoma hizi zilihamasisha mila na desturi katika jamii

Aidha ngoma hizi hutengenezwa kwa kutumia Ngozi za wanyama wanaofugwa katika jamii zetu na wakati mwingine huiingizia jamii kipatp kutoka na mauzo ya ngozi na ngoma zinazo tengenezwa.



 

mkuu wa mkoa wa kagera




Amani na maendeleo Kagera tuiendeleze