Ngoma hizo hupatikana katika miji ya watu binafsi ,ofisi za vijiji na katika majumba ya makumbusho mbalimbali yaliyopo hapa nchini kama vile BUDAP iliyopo eneo la Nyamkazi Bukoba Mjini,Bwera nyange Wilayani Karagwe ,Kiyanja, Kiziba, Kyamtwara Bujora Mwanza na sehemu nyinginezo hapa nchini zilizo kuwa ni Makao Makuu ya Machifu.
Tamaduni hizi zinapaswa kuendelezwa kwani jamii nyingi zimeanza kudharau tamaduni na kushabikia tamaduni za kigeni, kwani ngoma hizi zilihamasisha mila na desturi katika jamii
Aidha ngoma hizi hutengenezwa kwa kutumia Ngozi za wanyama wanaofugwa katika jamii zetu na wakati mwingine huiingizia jamii kipatp kutoka na mauzo ya ngozi na ngoma zinazo tengenezwa.
No comments:
Post a Comment