Saturday, March 24, 2012

MAUAJI YA ASKARI POLISI (W)BIHARAMULO

Na
Magreth Chaba
Biharamulo
WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wasiojulikana idadi mara moja wamemuua askari polisi katika machimbo ya Tulawaka katika eneo la Mavota Wilayani Biharamulo  kicha kumpora bunduki ikiwa na risasi zaidi ya 40 aliokuwa akitumia katika doria.
 Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Henry Salewi  amethibitisha kutokea kwa  tukio hilo  lilo tokea Machi 22, usiku wa kuamkia Machi 23, mwaka huu usiku.
Askari polisi aliyeuawa ametambuliwa kuwa ni PS konstebo  Dickson mwenye namba. G.2626 ambapo aina ya bundi alioporwa na watu hao ni Short gun mashine ambapo namba yake bado haijajulikana.
Kamanda Salewi alisema katika wauaji  hao walitumia chuma aina ‘Moke’ ambayo waliitumia kumtoboa nacho kichwani mara nne.
Alisema chuma hicho hutumika zaidi katika maeneo ya machimbo katika kuchimba ardhi.
Alisema siku ya tukio polisi huyo alikuwa na wenzake wanne ambapo kiutaratibu wakiwa malindoni hapo, huwagawanyika na hivyo kila mmoja kuangalia upande wake, ambapo kwa siku hiyo, wenzake waliingiliwa na shaka kwani hadi jana asubuhi hawakuweza kumwona akijitokeza.
Alisema kutokana na hali hiyo, walianza kumtafuta, ambapo walimkuta akiwa ameuawa kwa kutobolewa kichwani na chuma hicho mara nne.
Kamanda Salewi aliaeleza kuwa wauaji hao ni majambazi ambao jawajajulikana idadi hadi hivi sasa na haijaeleweka walikuwa na sialaha ya aina gani.
Alisema polisi hao walikuwa wakilinda ukuta wa jengo la machimbo la Tulawaka , ambapo mauaji hayo yalipomkuta askari huyo
Hata hivyo habari zaidi kutoka katika eneo la tukiko zinaeleza kuwa, watu waliohusika katika mauaji hayo ni Wachimbaji wadogo wa eneo hilo, siku ya tukio, Kostebo Dickson alienda kufanya doria usiku peke yake katika eneo hilo la machimbo lengo likiwa ni kuwazuia wachimbaji wadogo wanaojulikana eneo hilo kama Wangoni, ambao ni wavamizi wanaofahamika zaidi katiak eneo hilo kama wavamizi.
Kutokana na hali hiyo, haijaeleweka nia ya wangoni hao ilikuwa ni kutaka kumuua ama kumpora silaha.
Halikadhalika haijaeleweka kama costebo Dickson aliwataka watu hao wasiondoke na jiwe waliopata ama walitofautiana nini kati yao.
Kutokana na tukio hilo jana usiku wa kuamukia leo Jeshi la polisi lilitoa timu ya askari wapatao 40  wakiongozwa na baadhi ya maofisa wao kwenda katika eneo hilo la machimbo kufanya uchunguzi wa jambo hilo likiwa ni pamoja na kuwatafuta wauwaji na kuihakikisha linapata silaha ilioporwa ili isiweze kutumia mikononi mwa majambazi.
Tayari mwili huo umesafirishwa usiku wa kuamkia leo kwenda kwao Mkoani Rukwa  wilayani Sumbawanga kwa mazishi.
Katika machimbo la Mavota  ambayo yako ndani ya kijiji cha Mavota Kata Kiniha kinachomilikiwa na Kampuni ya Barrick  kumekuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya mauji, ambapo mara nyingi ni polisi kuuawa raia.
Mwaka 2009 polisi waliwauwa vijana watatu kwa kuwapiga kwa risasi kwa madai kuwa walivamia kituo cha polisi kwa kutaka kukiteketeza kwa moto, ambapo pamoja na mambo mengi ambayo yaharipotiwi hasa za mauaji wa raia yanapofanyiwa na polisi hao tetezi zilidai kuwa ni  vijana hao walienda kudai jiwe lao walionyang’anywa na polisi hao 

No comments:

Post a Comment