Tuesday, March 20, 2012

KESI YA KUPINGA MATOKEO BIHARAMULO


Na
Magreth Chaba

Kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Biharamulo
Magharibi, iliyoanza kusikilizwa Machi 14, mwaka huu katika Mahakama
ya Wilaya Biharamulo na Jaji Richard Kibela.

Imeendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo leo, ambapo upande wa
watoa maombi mlalamikaji namba moja Bw. Oscar Lwegasira Mkasa na
mlalamikiwa Mbunge wa Jimbo hilo Bw. Anthony Mbassa pamoja na
Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Wilaya ya
Biharamulo wameendelea kutoa ushahidi wao.

Akiwakilisha utetezi wake shahidi wa kwanza, Bw. Oscar Lwegasira Mkasa,
ambaye ni Mdai – akiongozwa na Wakili Aaron Kabunga mbele ya Jaji
Ridhard Kibela.

Shahidi huyo ameileza mahakama kuwa mnamo Oktoba 31-2010 katika
uchaguzi mkuu wa kitaifa, Rais, Bunge na Madiwani kuwa uchaguzi huo
katika Jimbo la Biharamulo Magharibi ulighubikwa na hira za makusudi,
Rushwa na udaganyifu.

Shahidi huyo ameileza mahakama kuwa, hila hizo zilifanywa na Chama cha
CHADEMA sambamba na Mawakala wake pamoja na tume ya Uchaguzi.
Kuandikisha watoto chini ya miaka 18, wapatao 2,325 walishiriki katika
zoezi la kupiga kura na kukipa ushindi Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA katika Jimbo hilo .

Aidha Shahidi huyo Bw. Mkasa amewakilisha maelezo 15 mbele ya Jaji wa
Mahakama hiyo Richard Kibela ambavyo vitatumika katika maombi ya kesi
yake.

Hata hivyo mahakama hiyo imetupilia mbali baadhi ya vielelezo baada ya
kusikiliza upande wa pili wa wajibu waombi ambao ulipinga kupokelewa
kwa baadhi ya vielelezo.

Vielelzo vilivyotupiliwa mbali na mahakama hiyo ni orodha ya majina ya
wapiga kura, fomu ya matokeo ya uchaguzi Kata ya Lunazi, Fomu ya
matokeo kituo cha Shule ya Msingi Kitwechembogo Kata ya Luziba
iliyodaiwa mahakamani hapo kuwa imeokotwa, Fomu kituo cha Kisuma,
(Kagondo stoo 2; na Kagondo mbili), ambavyo vituo havipo. (Vituo hivyo
vya Kagondo viko viwili kwa tofauti kama zilivyoainishwa).
kes hiyo imeahirishwa kusikilizwa hadi hapo kesho itakapo endelea kusikilizwatena huku upande wa mlalamika ukiendelea kutoa ushahidi wake.
 
 
 

No comments:

Post a Comment