Monday, November 26, 2012

M4C YAITESA CCM KARAGWE




Na: Magreth Chaba

Mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C) inayofanywa na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Wilayani Karagwe ikiongozwa na katibu Mkuu wa chama hicho Daktari Wilbroad Slaa imezoa makada zaidi ya 300 wa CCM na CUF.
Makada hao ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, na mjumbe wa mkutano Mkuu wa (CCM) kata ya kanoni Prince Bashaija  Rwazo ambaye pia ni mtoto wa katibu mwenezi wa (CCM) Mstaafu Mkoa wa Kagera na diwani wa kata ya Kanoni (CCM) Sabby Rwazo, na Mwenyekiti wa chama cha (CUF) kata ya Nyakahanga Enock Gabagambi ambao wamekabidhi kadi za vyama vyao vya zamani na kukabidhiwa kadi za (Chadema) na katibu wa chama hicho.

Ukiacha wanachama hao, zaidi ya wanachama 600 wamehama vyama vyao na kuhamia chadema, ambapo ilielezwa kuwa wanachama saba kutoka kata ya Nyakahanga  kupitia  Chama cha (CUF) wamekabidhi kadi za chama hicho na kuhamia chama cha demokrasia  na maendeleo (Chadema), kuwa pia wanachama 324 kutoka cham acha mapinduzi (CCM) wamekabidhi kadi zao.
Kwa mjibu wa katibu wa Chadema wilaya ya karagwe Geofrey Nguma alisema kuwa wanachama hao walitoka katika kata ya Nyakahanga, Kibondo, Nyakabanga na kata nyingine kuwa ni Bweranyange, Kiruruma, Nyabiyonza, RUGERA, Ihanda na Kayanga.
Aliongeza kuwa pamoja na baadhi ya makada hao waliokabidhi kadi zao kuwa zaidi ya wanachama wapya 600 wamejiunga na chama chake na kukata kadi ambapo katibu Mkuu wa chama hicho alishiriki kukabidhi kadi kwa wanachama hao.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana mjini Kayanga uliofanyika katika uwanja wa michezo mjini humo, muda mfupi baada ya katibu mkuu wa chedema kumkabidhi kadi Rwazo alisema ameamua kujiunga na chama hicho baada ya kuona chama cha mapinduzi hakina mwelekeo wa kuwasaidia watanzania tofauti na kuwanyanyasa na kukithiri kwa vitendo vya rushwa.
“Nimeona nihamie huku maana pamoja na kuwa kada mzuri wa CCM sioni mabadiliko yoyote zaidi ya majungu, rushwa na manyanyaso tunayotendewa na wenye chama nikiwa na maana ccm niyawachache wenye pesa ukitaka kuria akili kaa CCM” Alisema  Rwazo.

Kwa upande wake Kiongozi wa (M4C) kutika makao makuu ambaye pia ni katibu wa chadema Dodoma mjini Steven Massawe  aliwataka wananchi kuachana na CCM, kwani kwa miaka yote imeshindwa kuwaletea maendeleo na baadala yake wachukue hatua ili kuiondoa madarakani, vinginevyo vizazi vijavyo vitakuta mashimo. 

No comments:

Post a Comment