WAKRISTO GEITA WACHARUKA WADAI HAWAKO TAYARI KUCHOMEWA
MAKANISA
Na
MAGRETH CHABA
UMOJA wa makanisa ya kikristo ya Katoro wilayani Geita na
Buseresere wilayani Chato,mkoani Geita umecharuka na kulaani kitendo cha hivi
karibuni kilichofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu cha kuchoma
moto makanisa na kuharibu mali za wakiristo.
Kitendo hicho kilisababisha vurugu kubwa zilizotokea oktoba 12 mwaka huu Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam ambapo makanisa saba yalichomwa moto kutokana na kitendo kinachodaiwa na mtoto mwenye umri wa miaka 14 kukojolea Quran. Umoja huo umetoa tamko kuhusiana na kitendo hicho katika mkutano wa uliofanyika juzi mjini Katoro na kuwakutanisha waumini wa madhehebu mbalimbali ya kikristo pamoja na viongozi wao. Akitoa tamko hilo mwenyekiti wa umoja huo,Mchungaji Joseph Mwanzalima Hewa,alisema serikali ikishindwa kudhibiti matukio ya vurugu za waislamu kujichukulia sheria mkononi kutokana na udini taifa halitakuwa na amani. Alisema kuna hatari ya taifa,linaweza kuingia katika umwagaji wa damu kwani kitendo hicho hakivumiliki kwa wakristo kuzidi kupumbazika kwa kuharibiwa mali zao. Hewa alisema zaidi ya biblia 50 ziliwahi kuchomwa moto lakini wakristo hawakuchukua hatua zozote dhidi ya wahusika wala hakuna msikiti uliochomwa moto na kwamba hakuna vurugu zilizotokea na hivyo kuhoji uhalali wa waislamu kuiweka nchi kwenye rehani ya vita ya kidini. Alisema serikali inapaswa kuingilia kati kukomesha matukio hayo yanayofanywa na baadhi ya makundi ya waumini wa dini ya kiislamu ili nchi iendelee kuwa kisiwa cha amani. Aidha alisema kama serikali itashindwa kudhibiti matukio hayo,hawatavumilia kuendelea kuharibiwa makanisa yao na kudai kuwa wako tayari kufa wakitetea haki zao. Kiongozi huyo aliongeza kuwa waliohusika katika matukio hayo wanapaswa kuchukulia hatua kali za kisheria akiwemo kinara wa kikundi cha Uamsho kisiwani Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed. ''Serikali imekuwa ikiwakumbatia waislamu sasa tunasema yatosha,hatuwezi kuona mali zetu zinaharibiwa,kama itakuwa kimiya katika hili nchi itaingia katika vurugu kubwa na vita kutokana na udini ulioanza kujipenyeza''alisema Hewa. Naye aliyewahi kuwa mwenyekiti wa umoja huo Isaya Ikili alisema anasikitishwa na watendaji wa kata pamoja na viongozi wa serikali kushindwa kuhudhuria katika mkutano huo licha kupewa mwaliko ili kujua matamko yao. Alisema wako tayari kupambana na maadui wao wanaoharibu makanisa yao na kwamba polisi wasiingilie vurugu hizo kama serikali itashindwa kuyadhibiti. MWISHO. |
MW/KITI CCM GEITA APIGWA STOP MGODINI AKIENDA KUZINDUA
KAMPENI
|
No comments:
Post a Comment