Na Magreth Chaba.
MAMLAKA ya dawa na chakula
Tanzania [TFDA]imefunga duka la madawa katika hospitali teule ya wilaya ya
Biharamulo mkoani Kagera baada ya duka hilo kuendeshwa bila ya kuwa na mfamasia
wa kulihudumia.
Duka hilo limefungwa tangu Agosti
mwaka huu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wagonjwa wanaofika hospitalini
hapo ambao kutokana na hali hiyo wamekuwa wakilazimika kwenda kununua dawa
kwenye maduka ya watu binafsi.
Kwa mujibui wa mganga mkuu wa
hospitali hiyo Dk.Grasimus Sebuyoya,alisema duka hilo limejengwa kwa thamani ya
zaidi ya sh.12 milion na kwamba
limefungwa likiwa na dawa yenye thamani ya sh.30 millon.
Alisema kuwa uongozi wa hospitali hiyo
ulifikia uamuzi wa kuanzisha duka hilo kutokana na bohari ya dawa nchini[msd]
kushindwa kupeleka dawa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa ambao wamekuwa
wakisumbuka kwenda kununua dawa hizo nje ya hospitali hiyo.
Pia,Dk.Sebuyoya alisema lengo la
kuanzisha duka hilo ilikuwa kusaidia wagonjwa waliojiunga katika mifuko ya bima
ya afya CHF na NHIF kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wa kutafuta dawa Kutokana
na uhaba wa dawa kutoka Msd unaoikabili hospitali hiyo.
Alisema mamlaka ya dawa na chakula[TFDA]ilifunga
duka hilo kutokana na kukosa mfamasia wa kulisimamia.
‘’Tulipolianzisha tulitegemea
mfamasia wa halmashauri atakuwa msimamizi wa hilo duka lakini imekuwa
tofauti,tulivyokuwa tumetarajia na sisi hapa hatuna mfamisia wa kulisimamia
duka hilo,mpango uliopo tunatafuta mfamisia Atakayekithi kiwango ili
alisimamie,tuendeleze huu mradi wetu’’alisema Dk.Sebuyoya.
Aidha Dk.Sebuyoya aliongeza kuwa kutokana
na changamoto hiyo makundi maalumu hususa ni akina mama wajawazito,watoto chini
ya umri wa miaka 5,wazee na watu wenye magonjwa sugu wamekuwa wakilazimika
kununua dawa kwenye maduka ya watu binafsi kinyume na tamko serikali la kutoa kuhuduma
bure kwao.
‘’Serikali inasema tutoe huduma
kwa makundi hayo bure,lakini inashindikana,maana bohari wana muda mrefu
hawaleti dawa kwa maana hiyo tuna tatizo kubwa sana la ukosefu wa madawa na
sisi tuliamua kuanzisha duka hili ili tuwasaidie wagonjwa wawe wanapata dawa
karibu’’
Alisema hosiptali hiyo haijapokea
dawa kutoka bohari ya Taifa tangu mwezi wa tatu mwaka huu na kwamba hali hiyo
imekuwa ikiwalazimu wagongwa wanaofika katika hospitali hiyo wakiwemo watoto
chini ya miaka mitano,wajawazito,na wazee kwenda kununua dawa hizo mitaani.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment