Na
Magreth chaba
BIHARAMULO
HALI za
majeruhi waliolazwa katika Hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo kutokana na
ajali ya basi lilliloteketea kwa moto katika kijiji cha Nyantakala wilayani
Biharamulo mkoani Kagera zimeelezwa kuendelea vizuri huku mmoja kati yao akiwa
ameruhusiwa.
Mganga mkuu
wa hospitali hiyo Grasimus Sebuyoya amesema hali zao zinaendelea vizuri
ikilinganishwa na hali zao walipokuwa wanapokelewa katika hospitali hiyo.
Majeruhi
aliyeruhusiwa ametambulika kwa jina la Msigwa Isaya[22]mkazi wa Katoro mkoani
Geita ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kigoma.
Majeruhi wanaoendelea kupata matiobabu katika
hospitali hiyo ni Phinihas Elias[37]mwalimu wa shule ya sekondari Shamaliwa
Igoma jijini Mwanza,Pius John[21]askari wa JWT kikosi cha 24 kj Kigoma,Johary
Chapa[23]Mkazi wa Kwimba mkoani Mwanza,Josephina Ngereza[46]Kasulu ,Rashidi
Mahonda[48]Kasulu na Elies Ngereza[60]kazi
wa kasulu wote wakiwa wameungua moto sehemu mbalimbali za miili yao.
Majeruhi
wengine ni Dotto Tryphone[30]mkazi wa
Nyakanazi na Zainabu Issa(23)Mkazizi wa kigoma ambao wote wamevunjika miguu ya kushoto.
Ajali hiyo
ilitokea jana saa 4:30 asubuhi na kulihusisha basi la kampuni ya Adventure
lenye namba T 293 BDP Aina ya Nissani Diseal ambalo lilikuwa likitokea mkoani
Mwanza kwenda mkoani Kigoma.
Aidha Kamanda
wa polisi mkoa wa Kagera,Philip Kalangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni
kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme na kuongeza kuwa uchunguzi wa ajali
hiyo unaendelea.
Hata hivyo
kauli hiyo ya kamanda imetofautia na baadhi ya abiria wa basi hilo na mashuhuda
wa ajali ambao walisema huenda baadhi yao waliungulia ndani ya basi hilo hasa
watoto na wazee ambao walishindwa kujinusuru kutoka ndani ya basi hilo.
Kalangi alikanusha
madai ya kutokea Vifo katika ajali hiyo isipokuwa mali zilizokuwemo ziliteketea
kwa moto na kwamba abiria walionusurika katika ajali hiyo walisafirishwa na
basi jingine.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment