Na
Magreth
Chaba
BUKOBA
Zikiwa
zimesalia siku 3 kuuzika rasmi mwili Kardinali wa kwanza Afrika na askofu wa
kwanza Mwafrika Mwadhama Laurian Rugambwa ambaye alizikwa kwa muda katika
kanisa la Kashozi mwaka 1997, hatimaye atazikwa rasmi katika kanisa kuu jimbo
Katoliki la Bukoba, baada ya ukarabati wake kukamilika.
Askofu
msaidizi wa jimbo Katoliki la Bukoba Methodius Kilaini alisema kuwa maamuzi ya
marehemu Rugambwa kuzikwa Kashozi yalitokana na kanisa hilo alilochagua kuzikwa
kuwa katika ukarabati tangu mwaka 1996.
Askofu
Kilaini alisema kuwa mazishi hayo rasmi yatafanyika Oktoba 6 mwaka huu, siku
ambayo pia itakuwa ni kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Kardinali
Rugambwa ambaye alizaliwa mwaka 1912.
“Masalia
ya Kardinali Rugambwa yatahamishwa rasmi siku hiyo kutoka kanisa Katoliki la
Kashozi, tutasherehekea miaka 100 ya kuzaliwa kwake, lakini pia siku hiyo
Kanisa Katoliki jimbo la Bukoba litatabalukiwa” alisema.
Alisema
kitendo hicho ni kumbukumbu nzuri kwa Watanzania na Waafrika kwa ujumla
kutokana na kuwa Kardinali wa kwanza Afrika na Askofu wa kwanza Mwafrika,
hivyo wanategemea kupata wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi, na
kwamba baada ya mazishi hayo kanisa hilolitaanza kutumika
Alisema
kuwa baada ya shughuli hizo, kanisa Katoliki jimbo la Bukoba linataendelea kutumika
kwa ibada za kawaida, ili kuwaondolea
waamini wao adha ya kusalia katika holi.
“Tunaendelea
kuhamasisha waamini wetu wachangie fedha kwa ajili ya kumalizia sehemu ya
ujenzi iliyobaki, lakini pia wachangie sherehe hizo ili ziweze kufanyika kwa
ufanisi” alisema Askofu Kilaini.
Akizungumzia
historia ya Kardinali Rugambwa alisema kuwa alipewa Upadre mwaka 1943,
mwaka 1952 akapewa Uaskofu, mwaka 1960 akawa Kardinali na mwaka 1969 akawa
Askofu Mkuu Dar-Es-Salaam hadi alipostaafu mwaka 1992.
Akigusia
kidogo aliyoyafanya Kardinali Rugambwa ambayo baadhi yake yanawafanya watu waweke
kumkumbuka, Askofu Kilaini alisema kuwa
alianzisha kanisa kuu jimbo la Bukoba, alileta seminari kuu ya Ntungamo na
alijenga shule ya sekondari Rugambwa.
Mengine
ni ujenzi wa hospitali ya Mugana, kuanzisha vikoba kwenye parokia, kuanzisha
seminari ndogo ya Visiga na kuanzisha seminari kuu ya Segerea iliyoko
Dar-es-Salaam.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment