Monday, October 22, 2012

RAS GEITA:KISUKARI KINAHARIBU BAJETI YA SERIKALI.



RAS GEITA:KISUKARI KINAHARIBU BAJETI YA SERIKALI.

NA
Magreth Chaba

KATIBU tawala wa mkoa wa Geita,Severine Kahitwa amesema magonjwa ya kisukari,presha na ukimwi ni magonjwa ambayo yamekuwa yakiharibu mpango wa bajeti ya serikali kwa sababu magonjwa hayo hutibiwa kwa muda mrefu.

Alisema hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa magonjwa yasiyo ambukiza hapa nchini na kuwa tishio katika maisha ya binadamu kwa kupunguza muda wa kuishi na ubora wa maisha pamoja na kuathiri maendeleo ya Taifa.

Rai hiyo ilitolewa leo(jana) kwenye uzinduzi wa mradi wa afya ya jamii kwa wakazi wa mji wa Geita unaotekelezwa na shirika la Amref kwa ushirikiano na kampuni ya Mgodi wa Geita GGM na Halmashauri ya wilaya ya Geita.

Katibu tawala alisema magonjwa hayo yamekuwa tishio kubwa hapa nchini na kwamba serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuhudumia wagonjwa wanakumbwa na magonjwa hao na hivyo jamii kuitaka kuwa na tabia ya kijitokeza kupima afya kila wakati.

Akisoma hotuba yake alisema magonjwa hayo yamekuwa yakienea kwa kasi kutokana na mfumo wa maisha ambayo mtu huamua kuishi na hasa kuhusu vyakula anavyotumia,mazoezi ya mwili na kujijengea tabia zisizoaa kiafya.

Kufuatia hali hiyo,Kahitwa amewataka wananchi kuachana na vyakula vya kisasa vyenye mafuta mengi na badala yake kutumia vyakula vya asili ili kuondokana na hatari ya kukumbwa na magonjwa hayo ambayo yamekuwa yakitibiwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu.

Shirika la Amref kwa kushirikiana na kampuni ya mgodi wa Geita GGM na halmashauri ya wilaya ya Geita unatekeleza mradi huo unalenga kupima magonjwa mbalimbali yakiwemo yasiyo ya kuambukiza,kama kisukari,presha,ugonjwa wa kinywa na meno pamoja na magonjwa ya zinaa na ukimwi.

Kaimu ofisa mradi huo Potence Mhaya,akielezea mradi huo alisema katika hatua ya uzinduzi mradi huo utatekelezwa katika kata ya Kalangalala na Mtakuja kwenye kijiji cha Nyakabare na kwamba huduma hiyo itaendelea kutolewa kwenye kila kituo cha afya.

Hata hivyo baadhi ya watu waliojitokeza jana kwenye siku ya uzinduzi wameomba serikali kuboresha huduma ya afya na kuondoa tatizo la uhaba wa dawa ambalo licha ya wao kujitokeza kupima na kugudulika kuwa magonjwa dawa za matibabu changamoto kwao.
                                           MWISHO
                                                  

No comments:

Post a Comment