Sunday, October 21, 2012

FISI WAZIDI KULETA MADHARA KWA BINADAMU GEITA

FISI wamezidi kuleta madhara kwa binadamu katika mkoa wa Geita,kufuatia wanawake wawili wakazi wa Kitongoji cha Ndati kijiji cha Shabaka wilaya ya Nyang'hwale kunusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na wananyama hao waliovamia makazi yao usiku wa manane kisha kuwajeruhi vibaya,mwanamke mmoja akiachwa bila kiganja cha mkono.

Matukio hayo yametokea siku chache baada ya mtoto Hawa Baltazari(5)kukamatwa na kuliwa na fisi katika kijiji jirani cha Nyakato kata ya Nyanguku wilayani Geita saa moja usiku wa kuamkia septemba 21 mwaka huu.

Mtoto huyo alinyakuliwa na fisi akiwa anatoka kujisaidia umbali wa mita 50 kutoka nyumba ya bibi yake aitwaye Mariamu Bwegera(65) ambaye alikuwa akiishi na mtoto huyo enzi za uhai wake.

Wanawake hao ambao mmoja amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita wametambulika kwa majina ya Janeti Lukas(21)ambaye alijeruhiwa vibaya usoni,kichwani,Tumboni na kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto na Laurencia Lubatula(38)amejeruhiwa mkono wa kushoto kwa kukwaruzwa na kucha za wanayama hao.

Matukio ya kushambuliwa wanawake hao yametokea saa 8:30 usiku wa kuamkia octoba 16 mwaqka huu baada ya fisi hao kugonga milango kwa nguvu kisha kuingia ndani ya nyumba za  familia mbili tofauti kisha kuwashambulia wakati wanawake hao wakijihami kunusuru watoto wao wachanga wasiliwe na wanyama hao.

Akizungumza  Mwenyekiti wa kitongoji cha Ndati  Kamuli Mashauri alisema kabla ya kutokea kwa matukio hayo makundi ya fisi yamekuwa yakionekana mara kwa mara katika kijiji hicho wakitafuta chakula hasa nyakati za jioni
Naye majeruhi wa tukio hilo Janet Lukas aliye lazwa   wodi namba nane ya majeruhi   amesema kabla ya kushambuliwa,fisi huyo alimjeruhi mume wake mguuni na baada ya kukimbia kwenda kuomba msaada kwa majirani fisi huyo aliiingia ndani na kuanza kumshambulia huku akiwa amemkumbatia mtoto wake Pendo Ayubu mwenye umri wa miezi tisa ili asiliwe na fisi.

Fisi huyo aliuawa na babu yake na Janeti aliyefika kutoa msaada baada ya kumpiga kwa shoka kichwani.

kwa upande wake Mganga wa zamu katika hospitali ya wilaya Geita aliye zungumza na mwandishi wa habari hizi Dk.Adam Sijaona alisema wanawake walipokelewa wakiwa katika hali mbaya kutokana na majeraha ya kucha za wanyama hao lakini baada ya kupatiwa matibabu wanaendelea vizuri na kwamba mmoja wao ameruhisiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu.

Aidha mwanamke Raulencia Lubatula alijeruhiwa wakati akinusuru mifugo wake wasishambuliwa ambapo fisi huyo alikuwa ameuwa mbuzi wawili na kondoo mmoja.

Akithibisha kutokea kwa matukio hayo ofisa wanayama pori wa wilaya ya Geita na Nyang'hwale Samweli Mwita alisema kuzagaa kwa fisi hao kunatokana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya mistu baada ya watu kujihusisha na uchomaji wa mikaa,kupasua mbao kilimo na kukata magogo.

Amesema wanayama hao wanapokosa sehemu ya kujihifadhi hulazimika kuzagaa kwenye makazi ya watu wakitafuta chakula na maji na hivyo wanapokuwa katika hatua hiyo ndipo wamekuwa wakisababisha madhara hao.

Aidha amesema jumla ya watoto sita wenye umri wa kati ya miaka mitano na sita wamekufa baada ya kuuawa na fisi kwenye kata za Nyanguku,Busolwa,Kakora,Nayarugusu,Lwezera na Nyijundu katika kipindi cha kuanzia april hadi oktoba mwaka huu,huku fisi 20 wanaodaiwa kuhusika katika matukio hayo wameuawa na askari wa kuzuia ujangiri.

Top of Form
Bottom of Form


No comments:

Post a Comment