Na
Magreth Chaba
Biharamulo
MADIWANI
wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamelituhumu jeshi la
polisi wilayani humo kujihusisha na uharibifu wa mazingira baada ya kufumbia
macho vitendo vya uvushwaji wa mkaa na magogo ya miti(Mbilimbi) kinyume cha
sheria,ambapo mazao hayo husafirishwa na watu wanaosadikiwa wahamiaji haramu wa
nje ya nchi na kuyapeleka nchini Rwanda.
Askari
waliotuhumiwa ni wa kituo kidogo cha Nyakanazi wilayani humo ambapo wanadaiwa
kushirikiana na wavunaji haramu wa raslimali ya misitu kutoka nchini Rwanda
ambao huvusha mazao hayo kwa njia ya malori kupitia kizuizi kilichopo kwenye
kituo hicho cha polisi licha ya kujua wazi kuwa kufanya hivyo ni kuhujumu
uchumi wa taifa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya diwani wa kata ya Kalenge Gabriel Kakulu kutaka kujua
chanzo cha uharibifu mkubwa wa misitu katika msitu wa hifadhi ya taifa wa
Biharamulo upande wa kata ya Nyantakara ambapo eneo kubwa limeharibiwa vibaya
baada ya wavamizi wa ndani na nje ya nchi kuingia ndani yake kinyume cha sheria
na kujihusisha na ukataji miti ya kupasua mbao,uchomaji mkaa,kilimo na
uchimbaji madini.
Kutokana
na hali hiyo Kakulu alidai kutokuwa na imani na baadhi ya watendaji wa idara ya
misitu waliopo kwenye kata hiyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo
kushindwa kudhibiti uvushwaji wa mazao hayo kinyume cha sheria licha ya
mazao hayo kusafirishwa kupitia kizuizi cha polisi kilichopo jirani kabisa na
kituo kidogo cha Nyakanazi ambapo yamekuwa yakipelekwa nchini Rwanda pasipo
kutozwa ushuru hali inayopelekea halmashauri hiyo kupoteza mapato mengi kila
kukicha.
No comments:
Post a Comment