Thursday, June 14, 2012

WALIMU SENGEREMA WAPINGA UHAMISHO WA ADHABU

KATIKA hatua iliyo kinyume na kanuni,taratibu na sheria za utumishi wa umma,idara ya elimu msingi wilayani Sengerema mkoani Mwanza,imeingia katika mgogoro mkubwa na baadhi ya walimu kutokana na kuwapa uhamisho wa adhabu bila malipo baadhi yao kwa kile kilichodaiwa wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kisiasa kinyume na taratibu za kazi.
 
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya idara hiyo zilisema hatua hizo zimeanza kuchukuliwa kutokana na shinikizo la madiwani wa ccm,ambao wamekuwa wakiwatuhumu walimu hao kujihusisha na siasa mahali pakazi na wakati wa kazi,tuhuma ambazo zilifikishwa hadi kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza mhandisi,Evarist Ndikilo ambaye alitoa agizo kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Elinas Pallangyo kuwachukulia hatua walimu hao.
 
 Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao yasiandikwe ,baadhi ya walimu  walisema kuwa wameshangazwa na hatua hiyo ya uongozi wa wa idara ya elimu Sengerema kwa vile hakuna utaratibu unaoonyesha mwalimu au mtumishi kumhamisha bila malipo.
 
‘’Kisheria sisi..hatupaswi kuhama bila malipo…kama wanaudhibitisho kweli walikutukuta tunajihusisha na siasa madarasani ama ofisini..watupeleke mahakamani,mimi sihami,na kama kunifukuza kazini wanifukuze,niko ladhi kwenda kulima au kuuza mitumba na sio kujihamisha mwenyewe’’alisema mmoja wa walimu hao.
 
Ofisa utumishi wa halmashauri hiyo,Lusajo Ngabo,alisema hatua zilizoanza kuchukuliwa na idara ya elimu msingi za kuwahamisha walimu hao bila malipo kuwa ziko kinyume na utaratibu wa utumishi wa umma,huku akipinga kuwa hakuna uhamisho unaoitwa uhamisho wa adhabu .
 
Alisema kuwa hatua zilioanza kuchukuliwa na idara hiyo ni kinyume cha kanuni,sheria na taratibu za utumishi wa umma za kumhamisha mtumishi bila kumlipa stahiki zake ikiwa ni pamoja na fedha za usumbufu,huku akipinga kauli ya ofisa elimu msingi anayedai kuwa uhamisho huo ni uhamisho wa adhabu.
 
Alisema sheria namba 50 na 51 ya utumishi wa umma ya mwaka 2003 inafafanua kuwa mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanasiasa na kwamba ana uhuru wa kuwasiliana na viongozi wa chama chake isipokuwa hapaswi kuiba nyaraka za serikali na kuzipeleka kwa viongozi wake wa chama.
 
‘’Mtumishi hazuiriwi kuwa mwanasiasa…isipokuwa hatakiwi kujihusisha na siasa wakati wa kazi na mahali pa kazi,lakini anaweza kuwa na ushabiki wa chama chochote kile…kwa maana hiyo hatua hizi zilizoanza kuchukuliwa ni kinyume cha sheria za utumishi wa umma..na hakuna uhamisho unaoitwa uhamisho wa adhabu’’alisema Ngabo.
 
Hata hivyo ofisa utumishi huyo alikiri kupata taarifa za kuwepo kwa uhamisho huo na kumtaka ofisa elimu Juma Mwanjombe kumpa nakala ya barua za uhamisho huo jambo ambalo halijatekelezwa na hivyo kupinga kuwa hakuna uhamisho wa adhabu unaotokana na ushabiki wa kisiasa.
 
Aliongeza kuwa mtumishi atachukuliwa hatua kama atashiriki siasa wakati na mahala pa kazi na si vinginevyo na anapobainika kufanya hivyo atashitakiwa kwa kosa la kujihusisha na siasa wakati na mahala pa kazi,wala adhabu yake sio uhamisho.
 
Akizungumzia agizo la mkuu wa mkoa wa Mwanza alilolitoa mei 8,mwaka huu kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Sengerema Elnasi Pallangyo,la kuhakikisha anawabaini walimu wanaojihusisha na siasa,ofisa utumishi alisema mkuu wa mkoa ni mwanasiasa na kwamba kila hatua huhukuliwa kwa kufuata sheria kwani agizo hilo alipaswa kulitoa kwa maandishi ya barua.
 
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya ofisa elimu mei 17,mwaka huu kuwaandikia barua za uhamisho walimu 27 kati yao walimu saba wanadaiwa kujihusiha na siasa,huku walimu wengine 20 wanasemekana kuishi nje na vituo vyao vya kazi.
 
Uchunguzi uliofanywa na MWANDISHI wa habari hizi umebaini kuwa bali na walimu hao kukiri kuzipokea barua hizo za uhamisho wamegoma kuhama kwenda kwenye vituo walivyopangiwa hadi watakapolipwa fedha za uhamisho,ambapo wamepinga kauli ya ofisa elimu ya kwamba wao wanajihusisha na siasa.
 
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema ambaye pia ni ofisa elimu msingi wilaya hiyo Juma Mwanjombe akizungumzia sakata hilo alisema hilo ni agizo la madiwani na kwamba hawezi kulipuuza huku akisisitiza kwamba mwalimu atakayeshindwa kutekeleza atasimamishiwa mshahara wake.
 
Alisema hatua hizo ni kufuatia madiwani kubaini kuwa kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakitoroka vipindi vyao vya masomo na kwenda kwenye vijiwe vya kahawa na kuanza kuzungumzia masuala ya siasa kinyume na sheria za utumishi wa umma.                                              MWISHO

MADIWANI BIHARAMULO WALITUHUMU JESHI LA POLIS


Na
Magreth Chaba
 Biharamulo

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamelituhumu jeshi la polisi wilayani humo kujihusisha na uharibifu wa mazingira baada ya kufumbia macho vitendo vya uvushwaji wa mkaa na magogo ya miti(Mbilimbi) kinyume cha sheria,ambapo mazao hayo husafirishwa na watu wanaosadikiwa wahamiaji haramu wa nje ya nchi na kuyapeleka nchini Rwanda.
 
Askari waliotuhumiwa ni wa kituo kidogo cha Nyakanazi wilayani humo ambapo wanadaiwa kushirikiana na wavunaji haramu wa raslimali ya misitu kutoka nchini Rwanda ambao huvusha mazao hayo kwa njia ya malori kupitia kizuizi kilichopo kwenye kituo hicho cha polisi licha ya kujua wazi kuwa kufanya hivyo ni kuhujumu uchumi wa taifa.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya diwani wa kata ya Kalenge Gabriel Kakulu kutaka kujua chanzo cha uharibifu mkubwa wa misitu katika msitu wa hifadhi ya taifa wa Biharamulo upande wa kata ya Nyantakara ambapo eneo kubwa limeharibiwa vibaya baada ya wavamizi wa ndani na nje ya nchi kuingia ndani yake kinyume cha sheria na kujihusisha na ukataji miti ya kupasua mbao,uchomaji mkaa,kilimo na uchimbaji madini.
 
Kutokana na hali hiyo Kakulu alidai kutokuwa na imani na baadhi ya watendaji wa idara ya misitu waliopo kwenye kata hiyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo  kushindwa kudhibiti uvushwaji wa mazao hayo kinyume cha sheria licha ya mazao hayo kusafirishwa kupitia kizuizi cha polisi kilichopo jirani kabisa na kituo kidogo cha Nyakanazi ambapo yamekuwa yakipelekwa nchini Rwanda pasipo kutozwa ushuru hali inayopelekea halmashauri hiyo kupoteza mapato mengi kila kukicha.
 
Alisema halmashauri ya Biharamulo ilitarajia kukusanya shilingi Milioni tatu katika robo ya mwaka katika bejeti yake 2011/12 katika mapato yake ya ndani lakini kutokana na baadhi ya